JUMANNE YA 19 YA MWAKA
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Eze. 2:8 – 3:4Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.
Akaniambia, Mwanadamu, haya! Waendee wana wa Israeli, ukawaambie maneno yangu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 119:14, 24, 72, 103, 111, 131Mausi yako ni matamu sana kwangu.
Nimeifurahia njia ya shuhuda zako,
Kana kwamba ni mali mengi.
Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu,
Na washauri wangu.
K. Mausi yako ni matamu sana kwangu.
Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu,
Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
Mausia yako ni matamu sana kwangu,
Kupita asali kinywani mwangu.
K. Mausi yako ni matamu sana kwangu.
Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele,
Maana ndizo changamko la moyo wangu.
Nalifunua kinywa changu nikakweta,
Maana naliyatamani maagizo yako.
K. Mausi yako ni matamu sana kwangu.
Shangilio la Injili
Yn. 17:17Neno lako ndiyo kweli, Ee Bwana, ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.
Injili
Mt. 18:1 – 5, 10 , 12, 14Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni