Jumanne ya 1 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ebr 2:5–12Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake; akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 8:2, 5–9Umemtawaza Mwanao juu ya kazi ya mikono yako.
Wewe, Mungu, Bwana wetu,
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Mtu ni kitu gani hata umkumbuke,
Na binadamu hata umwangalie?
K. Umemtawaza Mwanao juu ya kazi ya mikono yako.
Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu;
Umemvika taji ya utukufu na heshima;
Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako.
K. Umemtawaza Mwanao juu ya kazi ya mikono yako.
Umevitia vitu vyote chiini ya miguu yake,
Kondoo, na ng’ombe wote pia,
Naam, na wanyama wa kondeni,
Ndege wa angani, na samaki wa baharini,
Na kila kipitiacho njia za baharini.
K. Umemtawaza Mwanao juu ya kazi ya mikono yako.
Shangilio la Injili
Ebr 4:12Neno la Mungu li hai tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.
Injili
Mk 1:21-28Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, akisema Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii! Habari zake zikaenea mara kotekote katika nchi zote kandokando ya Galilaya.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni