Alhamisi ya 2 ya Majilio
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 41:13-20Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu; mimi, Bwana, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.
Nitafunua vijito vya maji juu ya vilima, na chemchemi katikati ya mabonde; nitageuza jangwa kuwa ziwa la maji, na mahali pakavu kuwa vijito vya maji.
Nitapanda katika jangwa mwerezi, mshita, mhadasi, na mbono; nitatia katika nyika mberoshi, mtidhari, na mteashuri pamoja; ili waone, na kujua wakafikiri, na kufahamu pamoja, ya kuwa mkono wa Bwana ndio uliofanya jambo hilo. Mtakatifu wa Israeli ndiye aliyeliumba.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 145:1, 9-13Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema.
Ee Mungu wangu, Mfalme nitakutukuza,
Nitalihimidi jina lako milele na milele.
Bwana ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
K. Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema.
Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi,
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako.
K. Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema.
Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
K. Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema.
Shangilio la Injili
Isa 45:8Dondokeni, enyi mbingu toka juu, Mawingu yamwage haki; nchi na ifunuke, ili kutoa wokovu.
Aleluya.
Injili
Mt 11:11-15Mwenye masikio, na asikie.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni