Kumbukumbu ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ayu 19:21-27Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 27:7-9, 13-14Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai.
Ee Bwana, usikie, kwa sauti yangu ninalia,
Unifadhili, unijibu.
Uliposema, Nitafuteni uso wangu,
Moyo wangu umekuambia,
Bwana, uso wako nitautafuta.
K. Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai.
Usinifiche uso wako,
Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira.
Umekuwa msaada wangu, usinitupe,
Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
K. Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai.
Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana
Katika nchi ya walio hai.
Umngoje Bwana, uwe hodari,
Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.
K. Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai.
Shangilio la Injili
Yn 8:12Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
Injili
Lk 10:1-12Na nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni, ufalme wa Mungu umewakaribia. Na mji wowote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yentu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia. Nawaambia ya kwamba siku i8le itakuwa rahisi zaidi Sodomo kuistahimili adhabu ya mji huo.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni