Ijumaa ya 24 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Kor 15:12–20Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 17:1, 6–8, 15Nishibishwe, Ee Bwana, kwa sura yako.
Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu,
Utege sikio lako kwa maombi yangu,
Yasiyotoka katika midomo ya hila.
K. Nishibishwe, Ee Bwana, kwa sura yako.
Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,
Utege sikio lako ulisikie neno langu.
Dhihirisha fadhili zako za ajabu,
Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia;
Kwa mkono wako wa kuume
Uwaokoe nao wanaowaondokea.
K. Nishibishwe, Ee Bwana, kwa sura yako.
Unilinde kama mboni ya jicho,
Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
Bali mimi nikutazame uso wako katika haki,
Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.
K. Nishibishwe, Ee Bwana, kwa sura yako.
Shangilio la Injili
Efe 1:17, 18Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.
Injili
Lk 8:1–3Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
edwin msekalile · 18 Septemba 2020
aminaa.