Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Hes 21:4–9Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 78:1–2, 34–38Msiyasahau matendo ya Mungu.
Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu,
Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu.
Na nifunue kinywa changu kwa mithali,
Niyatamke mafumbo ya kale.
K. Msiyasahau matendo ya Mungu.
Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta;
Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii.
Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao,
Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wako.
K. Msiyasahau matendo ya Mungu.
Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,
Wakamwambia uongo kwa ndimi zao.
Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake,
Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.
K. Msiyasahau matendo ya Mungu.
Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema,
Husamehe uovu wala haangamizi.
Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake,
Wala haiwashi hasira yake yote.
K. Msiyasahau matendo ya Mungu.
Somo la Pili
Fil 2:6–11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
ShangilioEe Kristu tunakuabudu na kukutukuza, kwa kuwa umeikomboa dunia kwa msalaba wako.
Aleluya.
Injili
Yn 3:13–17Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni