Ijumaa ya 23 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Kor 9:16–19, 22–27Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 84:2–5, 7, 11Maskani zao zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Nafsi yangu imeziona shauku nyua za Bwana,
Naam, na kuzikondea.
Moyo wangu na mwili wangu
Ninamlilia Mungu aliye hai.
K. Maskani zao zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Shomoro naye ameona nyumba,
Na mbayuwayu amejipatia kioto,
Alipoweka makinda yanke,
Kwenye madhabahu zako, Ee Bwana wa majeshi,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
K. Maskani zao zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Heri wakaao nyumbani mwako,
Wanakuhimidi daima.
Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako,
Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.
Huendelea toka nguvu hata nguvu,
Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.
K. Maskani zao zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao,
Bwana atatoa neema na utukufu.
Hatawanyima kitu chema
Hao waendao kwa ukamilifu.
K. Maskani zao zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Shangilio la Injili
Mt 11:25Nakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya.
Injili
Lk 6:39–42Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni