Kumbukumbu ya Kukatwa kichwa kwa Yohane Mbatizaji
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Yer 1:17-19Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 71:1-6,15,17Kinywa changu kitasimulia haki yako.
Nimekukimbilia Wewe, Bwana,
Nisiaibike milele.
Kwa haki yako uniponye, uniopoe,
Unitegee sikio lako, uniokoe.
K. Kinywa changu kitasimulia haki yako.
Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,
Nitakakokwenda sikuzote.
Umeamuru niokolewe,
Ndiwe genge langu na ngome yangu.
Ee Mungu wangu, uniopoe mkononi mwa mkorofi.
K. Kinywa changu kitasimulia haki yako.
Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana Mungu,
Tumaini langu tokea ujana wangu.
Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa,
Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,
Ninakusifu Wewe daima.
K. Kinywa changu kitasimulia haki yako.
Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako,
Mchana kutwa; maana sijui hesabu yake.
Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu,
Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata milele.
K. Kinywa changu kitasimulia haki yako.
Shangilio la Injili
ShangilioHeri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Aleluya.
Injili
Mk 6:17-29Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya; ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalame akamwambia yule kijana, Niombe lolote utakaloniomba nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu. Basi akatoka, akamwuliza mamaye, Niombe nini? Naye akasema, Kichwa cha Yohane Mbatizaji. Mara akaingia kwa haraka mbele ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohane Mbatizaji. Mfalme akafanya huzuni sana lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia. Mara mfalme akatuma askari, akaamuru kuleta kichwa chake. Basi, akaenda, akamkata kichwa mle gerezani, akakileta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, naye yule kijana akampa mamaye. Wanafunzi wake waliposikia habari, walikwenda wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni