Kumbukumbu ya Mt. Augustino, Askofu na Mwalimu wa
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Kor 1:17–25Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandihsi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa. Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 33:1–2, 4–5, 10–11Bwana anajaza nchi na fadhili zake.
Mpigeni Bwana vigelegele, enyi wenye haki,
Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
Mshukuruni Bwana kwa kinubi,
Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
K. Bwana anajaza nchi na fadhili zake.
Kwa kuwa neno la Bwana lina adili,
Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
Huzipenda haki na hukumu,
Nchi imejaa fadhili za Bwana.
K. Bwana anajaza nchi na fadhili zake.
Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa,
Huyatangua makusudi ya watu.
Shauri la Bwana lasimama milele,
Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
K. Bwana anajaza nchi na fadhili zake.
Shangilio la Injili
Yn 17:17Neno lako ndiyo kweli, Ee Bwana, ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.
Injili
Mt 25:1–13Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni