Jumatano ya 14 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Hos. 10:1 – 3, 7 – 8, 12Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 105:2 – 7Siku zote mtafuteni uso wake Bwana.
Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini ajabu zake zote.
Jisifuni kwa jina lake takatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
K. Siku zote mtafuteni uso wake Bwana.
Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake sikuzote.
Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya.
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.
K. Siku zote mtafuteni uso wake Bwana.
Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake.
K. Siku zote mtafuteni uso wake Bwana.
Shangilio la Injili
2 Tim. 1:10Mwokozi wetu Yesu Kristo alibatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili.
Aleluya.
Injili
Mt. 10:1 – 7Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kodnoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni