Alhamisi ya 17 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 18:1–6Ndipo neno la Bwana likamjia, kusema, Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema Bwana. Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 146:1–5Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake.
Ee nafsi yangu umsifu Bwana,
Nitamsifu Bwana muda ninaoishi,
Nitamwimbia Mungu wangu ningali hai.
K. Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake.
Msiwatumainie wakuu,
Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake,
Siku hiyo mawazo yake yapotea.
K. Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake.
Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake.
Aliyezifanya mbingu na nchi,
Bahari na vitu vyote vilivyomo.
K. Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake.
Shangilio la Injili
1Pet 1:25Neno la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.
Injili
Mt 13:47–53Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Richard Chale · 31 Julai 2020
Naomba ikifika Ijumaa muweke masomo ya Jumamosi ili tujiandae kwa Jumuiya Ndogondogo mapema. Lengo ni kupata muda wa kutosha kutafakari tunapokutana asubuhi.