Kumbukumbu ya Mt. Marta, Mlei
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 15:10, 16–21Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao. Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema Bwana. Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 59:1–4, 9–10, 16–17Bwana ulikuwa ngome yangu siku ya shida yangu.
Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu,
Uniinue juu yao wanaoshindana nami.
Uniponye nao wafanyao maovu,
Uniokoe na watu wa damu.
K. Bwana ulikuwa ngome yangu siku ya shida yangu.
Kwa maana wanaiotea nafsi yangu;
Wenye nguvu wamenikusanyikia;
Ee bwana, si kwa kosa langu,
Wala si kwa hatia yangu.
Bila kosa langu huenda mbio, hujiweka tawari;
Uamke uonane nami, na kutazama.
K. Bwana ulikuwa ngome yangu siku ya shida yangu.
Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe,
Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu.
Mungu wa fadhili zangu atanitangulia,
Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu.
K. Bwana ulikuwa ngome yangu siku ya shida yangu.
Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi,
Nitaziimba fadhili zako kwa furaha.
Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu,
Na makimbilio siku ya shida yangu.
K. Bwana ulikuwa ngome yangu siku ya shida yangu.
Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha,
Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu,
Mungu wa fadhili zangu.
K. Bwana ulikuwa ngome yangu siku ya shida yangu.
Shangilio la Injili
Yak 1:21Pokeeni kwa upole neno la Mungu lililopandwa ndani liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.
Injili
Mt 13:44–46Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni