Alhamisi ya 12 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
2Fal 24:8–17Wakati ule watumishi wa Nebukadreza mfalme wa Babeli wakakwea kwenda Yerusalemu, na mji ukahusuriwa. Na Nebukadreza, mfalme wa Babeli akaufikilia huo mji, hapo watumishi wake walipokuwa wakiuhusuru. Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maakida wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
Akatoa huko hazina zote za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme, akavikatakata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani, mfalme wa Israeli, alivifanya katika hekalu la Bwana, kama Bwana alivyosema. Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi. Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maakida wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli. Na mashujaa wote, watu elfu saba, na mafundi na wafua chuma elfu moja, wote pia wenye nguvu, tayari kwa vita, hao wote mfalme wa Babeli aliwachukua mateka mpaka Babeli.
Mfalme wa Babeli akamtawaza Matania, ndugu ya baba yake, awe mfalme badala yake, akalibadili jina lake, akamwita Sedekia.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 79:1-5, 8–9Utuokoe, Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako.
Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako,
Wamelinajisi hekalu lako takatifu.
Wamefanya Yerusalemu chungu ngungu,
Wameziacha maiti za watumishi wako.
Ziwe chakula cha ndege wa angani.
Na miili wa watauwa wako
Iwe chakula cha wanyama wa nchi.
K. Utuokoe, Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako.
Wamemwaga damu yao kama maji
Pande zote za Yerusalemu,
Wala hapakuwa na mzishi.
Tumekuwa lawama kwa jirani zetu,
Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.
Ee Bwana, hata lini? Utaona hasira milele?
Wivu wako utawaka kama moto?
K. Utuokoe, Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako.
Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,
Rehema zako zije kutulaki hima.
Kwa maana tumedhilika sana.
K. Utuokoe, Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako.
Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,
Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe, utughfiri dhambi zetu,
Kwa ajili ya jina lako.
K. Utuokoe, Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako.
Shangilio la Injili
Zab 119:105Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
Injili
Mt 7:21–29Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni