Jumatano ya 12 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
2 Fal 22:8-13; 23:1-3Kisha, mfalme akatuma wajumbe, nao wakamkusanyia wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu. Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa Bwana, na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalemu, pamoja naye, na makuhani, na manabii, na watu wote, wadogo kwa wakubwa; akasoma masikioni mwao maneno yote ya kitabu cha agano kilichoonekana katika nyumba ya Bwana. Mfalme akasimama karibu na nguzo, akafanya agano mbele za Bwana, kumfuata Bwana, na kuyashika maagizo yake, na shuhuda zake, na amri zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kuyathibitisha maneno ya agano hilo yaliyoandikwa katika kitabu hicho; nao watu wote wakalikubali agano lile.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 119: 33-37, 40(K)Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako, Nami nitaishika hata mwisho.
(K)Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, Naam, nitaitii kwa moyo wangu wote.
(K)Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako, Kwa maana nimependezwa nayo.
(K)Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako, Wala usiielekee tamaa.
(K)Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako.
(K)Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Tazama, nimeyatamani mausia yako, Unihuishe kwa haki yako.
(K)Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Shangilio la Injili
Yn 15:4a, 5bKaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana.
Aleluya
Injili
Mt 7:15-20Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni