Jumanne ya 4 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
2Sam 18:9-10, 14, 24-25, 30–19:3Basi Daudi alikuwa ameketi kati ya malango mawili; mlinzi akapanda juu hata dari ya lile lango hata ukutani, akainua macho yake, akaangalia, na tazama, mtu anakuja mbio peke yake. Mlinzi akalia, akamwambia mfalme, Naye mfalme akasema, Kama yup eke yake, ana habari kinywani mwake. Akaja mbio, akakaribia. Naye mfalme akasema, Geuka, usimame hapa, Akageuka, akasimama.
Na tazama, yule Mkushi akafika; Mkushi akasema, Nina habari kwa bwana wangu mfalme; kwa maana Bwana amekulipizia kisasi leo juu ya hao wote walioinuka kupigana nawe. Naye mfalme akamwambia yule Mkushi, Yule kijana, Absalomu, je! Yu salama? Yule Mkushi akajibu, Adui za bwana wangu mfalme, na wote wainukao ili kukudhuru, na wawe kama alivyo yule kijana.
Naye mfalme akataabika sana, akapanda juu, akaingia kile chumba kilichokuwa juu ya lango, akalia; na katika kwenda kwake alisema hivi, Mwanangu Absalomu! Ee mwanangu! Mwangu Absalomu! Laity ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!
Kisha Yoabu akaambiwa, Angalia, mfalme anamlilia Absalomu na kumwomboleza. Na kushinda kwao vitani siku ile kukageuzwa kuwa maombolezo kwa watu wote; maana watu walisikia siku ule ya kwamba, Mfalme anahuzunika kwa ajili ya mwanawe. Watu wakajificha siku ile, wakaingia mjini kama vile watu waonao fedheha wajifichavyo, hapo wakimbiapo vitani.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 86:1-6Ee Bwana, utege sikio lako, unijibu.
Ee Bwana, utege sikio lako unijibu,
Maana mimi ni maskini na mhitaji.
Unihifadhi nafsi yangu, maana mimi ni mcha Mungu,
Wewe uliye Mungu wangu,
Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini.
K. Ee Bwana, utege sikio lako, unijibu.
Wewe, Bwana, unifadhili,
Maana nakulilia mchana kutwa.
Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako,
Maana nafsi yangu nakuinulia wewe, Bwana.
K. Ee Bwana, utege sikio lako, unijibu.
Kwa maana, Bwana, u mwema,
Umekuwa tayari kusamehe,
Na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao,
Ee Bwana, uyasikie maombi yangu,
Uisikilize sauti ya dua zangu.
K. Ee Bwana, utege sikio lako, unijibu.
Shangilio la Injili
Mt 8:17Mwenye aliutwaa udhaifu wetu, na kuyachukua magonjwa yenu.
Aleluya.
Injili
Mk 5:21–43Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya; aliposikia habari za Yesu, alipita katiak mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana, alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, anaye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.
Mara yesu, ahali akifahamu nafsi ni mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? Wanafunzi wake wakambwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa? Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo. Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. Akamwambia, Binti, Imani yako imekuponya, enenda zako kwa Amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
Hata laipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu? Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu. Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohane nduguye Yakobo. Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu. Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu. Wakamcheka sana.
Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana. Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka. Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana laikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu. Akawaonya sana, mtu asijue habari ile; akaamuru apewe chakula.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni