Jumanne ya 1 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
1 Sam 1:9-20Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
1 Sam 2:1, 4-5, 6-7,8Moyo wangu wamshangilia Bwana
Naye Hana akaomba, akasema,
Moyo wangu wamshangilia Bwana,
Pembe yangu imetukuka katika Bwana,
Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu;
Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;
K. Moyo wangu wamshangilia Bwana
Pinde zao mashujaa zimevunjika,
Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu.
Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula,
Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha.
Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba,
Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.
K. Moyo wangu wamshangilia Bwana
Bwana huua, naye hufanya kuwa hai;
Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha;
Hushusha chini, tena huinua juu.
K. Moyo wangu wamshangilia Bwana
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Humpandisha mhitaji kutoka jaani,
Ili awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu;
Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana,
Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
K. Moyo wangu wamshangilia Bwana
Injili
Mk 1:21-28Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni