Jumanne ya 6 ya Pasaka
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo 16:22-34Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 138:1-3, 7-8Utanyosha mkono, Ee Bwana, utaniokoa.
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,
Nitalishukuru jina lako,
K. Utanyosha mkono, Ee Bwana, utaniokoa.
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote.
Siku ile niliyokuita uliniitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
K. Utanyosha mkono, Ee Bwana, utaniokoa.
Na mkono wako wa kuume utaniokoa.
Bwana atanitimilizia mambo yangu;
Ee Bwana, fadhili zako ni za milele;
Usiziache kazi za mikono yako.
K. Utanyosha mkono, Ee Bwana, utaniokoa.
Injili
Yn 16:5-11Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni