Ijumaa ya 4 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ebr 13:1-8Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 27:1, 3, 5, 8-9Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu
Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu nani?
K. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu
Jeshi lijapojipanga kupigana nami,
Moyo wangu hautaogopa.
Vita vijaponitokea,
Hata hapo nitatumaini.
K. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu
Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya,
Atanisitiri katika sitara ya hema yake,
Na kuniinua juu ya mwamba.
K. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu
Bwana, uso wako nitautafuta.
Usinifiche uso wako,
Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira.
Umekuwa msaada wangu, usinitupe,
Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
K. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu
Shangilio la Injili
Zab. 130:5Roho yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.
Injili
Mk 6:14-29Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni