Jumatatu ya 3 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ebr 9:15, 24-28Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 98:1-6Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
K. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Bwana ameufunua wokovu wake,
Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka rehema zake,
Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.
K. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Mshangilieni Bwana, nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
K. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi,
Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
Kwa panda na sauti ya baragumu.
Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana.
K. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Shangilio la Injili
2Tim. 1:10Mwokozi wetu Yesu Kristu alibatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili.
Aleluya.
Injili
Mk 3:22-30Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni