Jumatatu ya 4 ya Majilio
· Mwaka C · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
2Sam. 7:1-5, 8-11, 16Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 89:1-4, 27, 29Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Fadhili za Bwana nitaziimba milele;
Kwa kinywa change nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Maana nimesema, fadhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.
K. Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Nimefanya agano na mteule wangu,
Nimemwapia Daudi, mtumishi wangu.
Wazao wako nitawafanya imara milele;
Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.
K. Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza;
Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia.
Wazao wake nao nitawadumisha milele,
Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.
K. Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Shangilio la Injili
ShangilioEe Utokaye Mashariki, Uliye mnga’ao wa mwanga wa milele na jua la haki, Njoo kuwaangazia wakaao gizani na katika kivuli cha mauti.
Aleluya.
Injili
Lk. 1:67-79Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni