Ijumaa ya 33 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ufu. 10:8 – 11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 119:14, 24, 72, 103, 111, 131Mausia yako ni matamu sana kwangu.
Nimeifurahia njia ya shuhuda zako,
Kana kwamba ni mali mengi.
Shuhuda zako ndizo furaha yangu,
Na washauri wangu.
K. Mausia yako ni matamu sana kwangu.
Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu,
Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
Mausia yako ni matamu sana kwangu,
Kupita asalai kinywani mwangu.
K. Mausia yako ni matamu sana kwangu.
Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele,
Maana ndizo changamko la moyo wangu.
Nalifunua kinywa changu nikatweta,
Maana naliyatamani maagizo yako.
K. Mausia yako ni matamu sana kwangu.
Shangilio la Injili
2Kor. 5:19Mungu alikuwa ndani ya Kristu, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Aleluya.
Injili
Lk. 19:45-48Naye akawa akifundisha kila siku hekaluni. Lakini wakuu wa makuhani, na waandishi, na wakuu wa watu walikuwa wakitafuta njia ya kumwangamiza; wasione la kutenda, kwa kuwa watu wote walikuwa wakiandamana naye, wakimsikiliza.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni