Jumatano. 04 Februari. 2026

Mt. Karoli Lwanga na wenzake

Karoli Lwanga na wenzake

Wafiadini hawa ishirini na wawili wote ni Waafrika. Walipata taji la mbingu wakati wa dhulumu ya Mwanga, mfalme wa Uganda, kati ya miaka ya 1885-1887. Alipokuwa kijana; Mwanga alipendelea sana kusikia mafundisho ya mapadre, alianza kuyaacha mambo yote ya kipagani, akawashauri watu wake wote waende kwa mapadre kufundishwa dini ya Yesu Kristu. Aliwachagua wakristu wengi akawapa kazi bora zilizokuwa chini ya uwezo wake.

Wajumbe na raia wapagani walipoona kuwa mfalme wao anakataa mambo yao kipagani, walipatana kwa faragha ili wamwue. Lakini siri yao ikajulikana kwa wakristu watatu waliokuwa watumishi wake. Mwanga aliwaita Katikiro (ndiyo Waziri Mkuu) na wengine waliofanya shauri la kumwua. Lakini walipotubu kosa lao aliwasamehe.

Toka siku hiyo Katikiro, wazee na wafumu walikula njama kuwaua wakristu. Kila siku walikwenda kwa mfalme Mwanga kuwashitaki kwa kumdanganya na kumwogofya. Kisha Mwanga alianza kudanganywa na mali na furaha mbaya za dunia; aliwashurutisha baadhi ya wakristu watende naye mabaya, lakini walikataa kishujaa kutenda hayo. Hapo Mwanga aliwakasirikia, akataka kuwaua.

MATIASI MULUMBA alikuwa jumbe na kiongozi wa wazee mashauri. Baba yake alipokuwa mzee alimwambia: "Watakuja watu weupe na wataleta dini mpya. Utakapowaona uwapokee vizuri na uwasadiki".

Waarabu walipofika Uganda Mulumba aliwafuata. Lakini baada ya miaka michache wamisionari Waprotestanti walikuja huko Uganda. Mulumba aliyasikia mafundisho yao, akayasadiki. Alipokuwa karibu kubatizwa, walikuja wamisionari Wakatoliki. Alipoyasikia mafundisho yao maya mbili, roho yake ikapata nuru, akajisikia ndani yake furaha kuu ambayo alikuwa hajaiona bado katika dini nyingine. Toka siku ile alifuata vema mafundisho ya Mapadre na tarehe 28 Mei 1882 alibatizwa pamoja na mkewe. Baada ya kubatizwa aliwafundisha watoto wake ili nao wawe wakristu, Alipendwa sana na watu wengine. Alijenga nyumba ya kulala kwa ajili ya watu wa mbali, ili wapate kuja kwenye mafundisho, na mara kwa mara aliwapa chakula. Alipokamatwa na wauaji aliungama kwa uhodari dini yake. Alikatwa mikono, miguu, nyama ya mgongo na ile ya kifuani, lakini hakulia hata kidogo. Aliomba Mungu akisema: "Ee Mungu wangu, Mungu wangu". Shahidi huyo alikufa tarehe 28 Mei 1886. Mungu aliwazuia wanyama wa porini na ndege waiguse maiti ya mtumishi wake mwaminifu. Hivyo baada ya siku chache mapadre walikuja kuuchukua mwili wake wakauzika.


KAROLI LWANGA alikuwa kijana hodari, na wakati huo akiwa na umri wa miaka ishirini. Mfalme alimpenda kwa sababu alimwona ni mzuri, hodari, na pia alikuwa na tabia njema. Alimfanya msimamizi wa vijana mia tatu. Karoli aliwatangulia vijana wengine kusikiliza mafundisho ya mapadre, na vijana wengine walimfuata wakabatizwa. Mwanga aliposhikwa na tamaa mbaya za mwili alitaka kuwashawishi wale vijana kumridhia katika tamaa zake chafu. Karoli aliwasaidia vijana kujificha ili wapate kukaa na moyo safi. Aliwasaidia pia walipokamwatwa, hata aliwabatiza gerezani vijana wanne waliokuwa bado wakatekumeni.

Siku moja asubuhi, kwa amri ya Mwanga, Karoli aliwakusanya vijana wote. Hapo Mwanga aliwaambia: "Kati yenu wale ambao hawataki kusali na kufuata dini ya kikristu wakae hapa karibu nami, na wale wanaotaka kusali na kufuata "

Maoni


Ingia utoe maoni