Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Kufafanua Alama za Nyakati Zetu!

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Ijumaa ya 29 ya Mwaka → Efe 4:1–6 · Zab 24:1–6 · Lk 12:54-59
Injili ya leo kutoka kwa Mt. Luka, inatuelezea ni kwa jinsi ghani watu wakipindi cha Yesu walivyokuwa wiweza kufafanua majira na nyakati zao, kutambua uso wa nchi na mbingu, lakini walishindwa kutambua alama za Yesu alizoweka mbele ya macho yao katika kutangaza Ufalme wa Mungu. Je, si kweli zaidi hata kwetu sasa? Tumebobea sana katika teknologia na tunajivuna katika hali ya ukuwaji wa sayansi tuliofanya kama jamii, lakini mara nyingi tunakosa ujumbe wa Mungu anaojaribu kuwasiliana nasi kila siku.

“Alama za nyakati” ilikuwa ni ujumbe muhimu katika mkutano wa pili wa Vatikan, kama ulivyotutaka kuelezea ujumbe wa Mungu katika alama za nyakati zetu, na pia kubaki katika ukweli wa ujumbe wa Yesu na habari njema iliohubiriwa na Mababa wa kanisa. Wakati watu wanaongelea kuhusu siasa, michezo au dini, mara nyingi midahalo ni ya kutumia nguvu nyingi na hisia. Lakini tunapoulizwa ni nini mpango wa Mungu katika maisha yetu, wengi wetu twaweza kusema hatujui. Mara nyingi hatuna uhakika na anacho tuambia Mungu tufanye katika maisha yetu, tofauti na mipango yetu na tamaa zetu. Mara nyingi tunajifanya na kupotea huku tukijifanya hamna chochote kibaya kwa uchaguzi wetu na maamuzi yetu; kwa kifupi, inatuwia vigumu kubadilika. Mt. Paulo katika somo la kwanza anawaandikia Waefeso akiwaeleza kuwa wajiandae kushika mambo ya msingi kwa kushika njia sahihi. Waenende kadiri ya wito wao walioitiwa na Mungu.

Sala:
Bwana, tusaidie leo, ili tuweze kuelezea kwa usahihi neno lako kwa njia ya alama za nyakati zetu.
Amina
0 Maoni

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni