Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Upendo wa Agape!

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Kumbukumbu ya Mtakatifu Karoli Lwanga na Wenzake → 2Tim 1:1-3, 6-12 · Zab 123:1-2 · Mk 12:18-27
Kwakusoma Injili tunaweza kufanya muktasari wa nafsi ya Yesu kwa neno moja tu, nalo ni UPENDO. Yesu anatuambia kwamba sheria zote zinaweza kufupishwa katika sheria mbili tuu. Ya kwanza kabisa ambayo ni muhimu sana ni upendo kwa Mungu usio na kikwazo chochote, ya pili ni matokea ya hiyo ya kwanza, kwasababu wakati mwanadamu anapendwa, Mungu anapendwa, kwasababu mwanadamu ameumwa kwa sura na mfano wa Mungu

Upendo ulimsukuma Yesu aweze kuwanyanyua wanyonge, kuwasaida waliotengwa, kuponya walioumizwa, kuwafanya huru wafungwa na akatoa maisha yake msalabani ili kutukomboa sisi kutoka utumwa wa dhambi. Upendo wa Mungu hauna masharti. Yesu kwa maneno na matendo yake anatuhimiza kutimiza na kutenda “UPENDO huu” kwaajili ya ukombozi wetu na ukombozi wa ulimwengu mzima. Na hiki ndicho kitambulisho chetu kama Wakristo wanaomfuata Yesu kwa uaminifu. Kwa namna hiyo tutakuwa wakristu wa kweli “kama Kristo”. Pengine tujiulize swali lingine ambalo hatujazoea sana kujiuliza, tunajua Mungu anatupenda wote bila ubaguzi. Je, ninampenda mwenzangu/jirani yangu kama Mungu anavyompenda?

Sala:
Bwana; nisaidie niweze kuwa Mkristo wa kweli kwa kuishi na kutimiza Upendo usio na masharti wala kikomo.
Amina.
0 Maoni

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni