Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
← Sala zote
Sala

Kanuni ya Imani ya NICEA

Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi Mwumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu,mwana wa pekee wa Mungu. Aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote. Mungu aliyetoka kwa Mungu,mwanga kwa mwanga,Mungu kweli kwa Mungu kweli. Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba, ambaye vitu vyote vimeumbwa naye. Ameshuka toka mbinguni kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu. Akapata mwili kwa uwezo wa roho mtakatifu kwake yeye Bikira Maria akawa mwanadamu. Akasulibiwa pia kwa ajili yetu sisi Akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,akafa akazikwa. Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa. Akapaa mbiguni, amekaa kuume kwa baba Atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu nao ufalme wake hautakuwa na mwisho Nasadiki kwa Roho Mtakatifu Bwana mleta uzima atokaye kwa Baba na Mwana anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana aliyenena kwa vinywa vya manabii. Nasadiki kwa Kanisa moja,Takatifu Katoliki la mitume Naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi. Nangojea na ufufuko wa wafu. Na uzima wa milele ijayo. Amina.
3 Maoni

Maoni (3)

Loberei Araule · 3 Septemba 2023

Nahitaji PDF ya hii kanuni

DAVID ELIA · 22 Novemba 2024

Mahana ya PDF ni nini?

Donata Musa · 7 Julai 2026

Tumsifu yesu kristo mtot wa mungu

APONIUS AUDAX · 24 Mei 2026

weka na vitabu vya watakatifu na mawaridi ya sala pia.

Donata Musa · 7 Julai 2026

Ndugu zangu kunaswal 1.hekima ni nn?

Ingia utoe maoni