Sala ya Usiku
Kwako Mungu napandisha,
moyo wangu kwa shukrani,
nipumzike kwa amani,
Mema mengi umenipa,
ninashindwa kukulipa,
Baba mwema ondolea,
yote niliyokosea.
Yesu mpenzi unijie,
ombi langu usikie,
unifiche mtoto wako,
ndani ya jeraha zako,
Ewe Mama unipe neema,
raha na usiku mwema,
Roho mlizi ukakeshe,
pepo wasinikoseshe
Naiweka roho yangu,
mikononi mwa Baba yangu,
bila hofu napumzika,
mwisho kwake nitafika.
Amina
Maoni (12)
Elia Stanley Mlay · 5 Juni 2020
Ee Mungu naomba usiku huu ninapoenda kulala ukanikinge na pepo wachafu,majinamizi,wachawi,vibwengo ,nilale salama pamoja na watoto wangu sita AMEN
Andrew Timotheo · 31 Machi 2023
Ee MUNGU mwingi wa rehema na baraka uturinde usiku huu mimi na familia yangu utupe usingizi mnono mikononi mwako vichwa vyetu twajilaza wewe uu mkuu leo hata milele Amina
Joseph Marekani · 15 Machi 2024
Ee mungu nibaliki tunapo enda kulala maraika mlinzi awe pamoja nasi na tuamke na fulaha na upendo amina
Marekani Nestory · 18 Machi 2024
Mungu wangu wabaliki watu ote wanao fuatilia mkatoliki leo walale salama na waamke wenyenguvu na afya tele amina
GASPER MKELEMI · 12 Novemba 2024
amina
DAVID ELIA · 21 Novemba 2024
Hacha mungu akubariki sisi zote katika usiku ya leo
Leokadia Pius · 26 Februari 2025
Hii sala ni nzuri sana ndugu wakristo wenzangu unapaswa kumshuru mungu kwa yote aliyokutendea toka asubuhi mpak jion
Donata Musa · 8 Julai 2026
Mm kila ck jion namshukulu mungu mwenyezi
Ngelela. Ngusa. · 5 Juni 2025
Mungu ni wetu sote,hivyo tujitahidi kuwashauri wasiomjua mungu wamjue kwani ndio msaada na kimbilio letu wanadamu.Amina.
fulugenzi mapunda · 5 Novemba 2025
asande mungu
fulugenzi mapunda · 6 Novemba 2025
Sasande mungu wangu
Donata Musa · 8 Julai 2026
Tusal kila ck jaman wapenz wa mungu sala za asubuhi na za jion
Kamgisha Elipidius · 29 Julai 2026
Mungu wangu huturinde usiku huu wa leo ilinde familly yangu waponye wagonjwa waliopo majumbani na huko hospitari bwana niongoze kwenye kazi zangu ubavuni mwako nifiche adui zangu wasinipate mungu shusha maraika wako watuzingire mahari hapa bwana nashukru haya machache uliyonipatia naomba hayo kwa jina la mwanao kipenzi yesu kristo. amen