Kumbukumbu ya Malaika Walinzi
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Kut. 23:20-23Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 91:1-6.10-11Amekuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote.
Aketiye mahali pa siri pake aliye juu,
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
K. Amekuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote.
Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,
Na katika tauni iharibuyo.
Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio.
K. Amekuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote.
Hutaogopa hofu ya usiku,
Wala mshale urukao mchana,
Wala tauni ipitayo gizani.
Wala uele uharibuo adhuhuri,
K. Amekuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote.
Mabaya hayatakupata wewe,
Wala tauni haitaikaribia hema yako.
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake
Wakulinde katika njia zako zote.
K. Amekuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote.
Shangilio la Injili
Mt. 18:1-5,10Mhimidini Bwana, enyi majeshi yake yote, ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.
Aleluya.
Injili
Mt. 18:1-5.10Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni