KUMBUKUMBU YA MT. GREGORI MKUU (Papa)
· Mwaka B
Somo la Kwanza
1 Kor. 2:1 – 5Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 119:97 – 102Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu.
Sharia yako naipenda mno ajabu,
Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.
Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu,
Kwa maana ninayo siku zote.
K. Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu.
Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote,
Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.
Ninao ufahamu kuliko wazee,
Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
K. Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu.
Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya,
Ili nilitii neno lako.
Sikujiepusha na hukumu zako,
Maana Wewe mwenyewe umenifundisha.
K. Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu.
Shangilio la Injili
Kol. 3:16, 17Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote; mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Aleluya.
Injili
Lk. 4:16 – 30Akakifunga chuo, akamtudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake.
Wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu? Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende hapa pia katika nchi yako mwenyewe. akasema, Amin, nawaambia ya kuwa, Hakuna nabii mwenye kukubalika nchi yake mwenyewe. Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitano na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu. Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo. Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini; lakini yeye alipita katikati yao, akaenda zake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni