Kumbukumbu ya Mt. Dominiko
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer. 31:1–7Bwana asema hivi, Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha. Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu. Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli, mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi. Mara ya pili utapanda mizabibu juu ya milima ya Samaria; wapanzi watapanda, nao watayafurahia matunda yake. Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni tukaende Sayuni, kwa Bwana, Mungu wetu.
Maana Bwana asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkasema, Ee Bwana, uwaokoe watu wako mabaki ya Israeli.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Yer. 31: 10–13Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Lisikieni neno la Bwana,
Enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali,
Mkaseme Aliyemtawanya Israeli atamkusanya,
Na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Kwa maana Bwana amemweka huru Yakobo,
Amemkomboa mkononi mwake
Aliyekuwa hodari kuliko yeye.
K. Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni,
Wataukimbilia wema wa Bwana, nafaka, na divai;
Na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng’ombe
Na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji;
Wala hawatauzunika tena kabisa.
K. Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Ndipo bikira atafurahi katika kucheza,
Na vijana na wazee pamoja;
Maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha,
Nami nitawafariji,
Na kuwafurahisha waache huzuni zao.
K. Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Shangilio la Injili
Zab. 119: 105Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
Injili
Mt. 15:21–28Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni