Kumbukumbu ya Mt. Yohane Maria Vianney
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer. 26:11–16, 24Ndipo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani, na manabii, wakisema, Mtu huyu hastahili kuuawa; kwa maana amesema nasi katika jina la Bwana, mungu wetu. Mkono wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ulikuwa pamoja na Yeremia, wasimtie katika mikono ya watu auawe.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 69:14–15, 29–30, 32–33Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Mungu.
Uniponye kwa kunitoa matopeni,
Wala usiniache nikazama.
Na niponywe nao wanaonichukia,
Na katika vilindi vya maji.
Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze,
Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
K. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Mungu.
Nami niliye maskini na mtu wa huzuni.
Mungu, wokovu wako utaniinua.
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani.
K. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Mungu.
Walioonewa watakapoona watafurahi,
Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji,
Wala hawadharau wafunga wake.
K. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Mungu.
Shangilio la Injili
Zab. 119:18Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.
Aleluya.
Injili
Mt. 14:1–12Maana Herode alikuwa amemkamata Yohane, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye. Kwa sababu Yohane alimwambia, Si halali kwako kuwa naye. Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohane kuwa nabii. Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Heorode. Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lolote atakaloliomba. Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohane Mbatizaji. Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; akatuma mtu akamkata kichwa Yohane mle gerezani. Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye. Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni