Jumatatu ya 17 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer. 13:1–11Hata ikawa baada ya siku nyingi, Bwana akaniambia, Ondoka, enenda mpaka mto Frati, ukautwae ule mshipi, niliokuamuru kuuficha huko. Ndipo nikaenda mpaka mto Frati, nikachimba, nikautwaa ule mshipi katika mahali pale nilipouficha; na tazama, mshipi ulikuwa umeharibika, haukufaa, tena kwa lolote. Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema, Bwana asema hivi, Jinsi iyo hiyo nitakiharibu kiburi cha Yuda, na kiburi kikuu cha Yerusalemu. Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wanaokwenda kwa ushupavu wa mioyo yao, na kufuata miungu mingine ile kuitumikia na kuiabudu, watakuwa hali moja na mshipi huu, usiofaa kwa lolote. Maana kama vile mshipi unavyoshikamana na viuno vya mtu, ndivyo nilivyowashikamanisha nami nyumba yote ya Israeli, na nyumba yote ya Yuda, asema Bwana; wapate kuwa watu kwangu mimi, na jina, na sifa, na utukufu; lakini hawakutaka kusikia.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Kumb. 32:18–21Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa.
Hukumbuki Mwamba aliyekuza,
Mungu aliyekuzaa umemsahau.
Bwana akaona, akawachukia,
Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake.
K. Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa.
Akasema, nitawaficha uso wangu,
Nitaona mwisho wao utakuwaje;
Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi,
Watoto wasio imani ndani yao.
K. Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa.
Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu,
Wamenikasirisha kwa ubatili wao;
Nami nitawatia wivu kwa wasio watu.
Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.
K. Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa.
Shangilio la Injili
ShangilioNeno la Kristu likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkimshukuru Mungu Baba kwa Yeye.
Aleluya.
Injili
Mt. 13:31–35Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni