Jumanne ya 11 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
1 Fal. 21:17-29Ahabu akamwambia Eliya, Je! Umenipata, ewe adui yangu? Akamwambia, Nimekupata, kwa sababu umejiuza utende yaliyo mabaya machoni pa Bwana. Angalia, nitaleta mabaya juu yako; nami nitakuangamiza kabisa, nitamkatia Ahabu kila mume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli.
Kisha nitaifanya nyumba yako iwe kama nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebari, na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya, kwa ajili ya chukizo ulilonichukiza, hata kunighadhibisha, ukawakosesha Israeli. Tena Bwana alinena habari za Yezebeli, akisema, Mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli. Mtu wa nyumba ya Ahabu afanye mjini, mbwa watamla, na yeye afaye mashamba ndege wa angani watamla.
Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana, ambaye Yezebeli mkewe alimchochea. Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.
Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole. Neno la Bwana likaja kwa Eliya Mtishbi, kusema, Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu? Basi kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katik asiku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 51:1-4, 9, 15Ee Mungu uturehemu uyafute makosa yetu.
Ee Mungu unirehemu, sawasawa na fadhili zako.
Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu.
Unioshe kabisa na uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu.
K. Ee Mungu uturehemu uyafute makosa yetu.
Maana nimejua mimi makosa yangu,
Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
Nimekutenda dhambi Wewe peke yako.
K. Ee Mungu uturehemu uyafute makosa yetu.
Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu,
Uzifute hatia zangu zote.
Ee Bwana, uifumbue midomo yangu,
Na kinywa hcangu kitazinena sifa zako.
K. Ee Mungu uturehemu uyafute makosa yetu.
Shangilio la Injili
Yak. 1:21Pokeeni kwa upole neno la mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuiokoa roho zenu.
Aleluya.
Injili
Mt. 5:43 – 48Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni