Kumbukumbu ya Moyo Safi wa Bikira Maria
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Isa. 61:9-11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
1 Sam. 2:1, 4-8Moyo wangu wamshangilia Bwana.
Moyo wangu wamshangilia Bwana,
Pembe yangu imetukuka katika Bwana,
Kinywa change kimepanuka juu ya adui zangu;
Kwa kuwa naufurahia wokovu wako.
K. Moyo wangu wamshangilia Bwana.
Pinde zao mashujaa zimevunjika,
Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu.
Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula,
Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha.
Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba,
Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.
K. Moyo wangu wamshangilia Bwana.
Bwana huua, naye hufanya kuwa hai;
Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha;
Hushusha chini, tena huinua juu.
K. Moyo wangu wamshangilia Bwana.
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Humpandisha mhitaji kutoka jaani,
Ili awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu.
K. Moyo wangu wamshangilia Bwana.
Injili
Lk. 2:41-51Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia.
Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake. Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni