Sikukuu ya Maamkio ya Bikira Maria
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Rum. 12:9-16Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafuraio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Isa. 12:2-6Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana Bwana Yeshova ni nguvu zangu na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
K. Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,
Litajeni jina lake kuwa limetukuka.
K. Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Mwimbieni Bwana; kwa kuwa ametenda makuu;
Na yajulikane haya katika dunia yote.
Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
K. Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Shangilio la Injili
Lk. 1:45Heri Bikira Maria aliyesadiki ya kuwa aliyoambiwa na Bwana yatatimizwa.
Aleluya.
Injili
Lk. 1:39-56Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa; Kwa kuwa mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwa hao wanaomcha. Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao; Amewaangusha wakuu katika ivti vyao vya enzi; na wanyonge amewakweza. Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele. Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni