Sikukuu ya Bwana Wetu Yesu Kristo Kuhani Mkuu Mile
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer. 31: 31 - 34Israeli, na nyumba ya yuda. Si kwa mfano wa agano lilenililofanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.
Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana: Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika. Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema: Mjue Bwana, kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maananitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 109:1a-e, 2,3Ndiwe Kuhani hata milele kwa mfano wa Melkisedeki.
Neno la Bwana kwa Bwana wangu,
Uketi mkono wangu wa kuume,
hata niwafanyapo adui zako
kuwa chini ya miguu yako.
K. Ndiwe Kuhani hata milele kwa mfano wa Melkisedeki.
Bwana atainyosha toka Sayuni
fimbo ya nguvu zako,
Uwe na enzi juu ya adui zako!
K. Ndiwe Kuhani hata milele kwa mfano wa Melkisedeki.
Watu wako watajitoa kwa hiari,
siku ya uwezo wako;
kwa uzuri wa utakatifu,
tokea tumbo la asubuhi,
unao umande wa ujana wako
K. Ndiwe Kuhani hata milele kwa mfano wa Melkisedeki.
Somo la Pili
Ebr 10: 11 -18“Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana: Nitatia sheria zangu mioyoni mwao; na katika nia zao nitaziandika; Ndipo anenapo, Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Ebr 5:8 9Ingawa ni Mwana alijifunza kutii, kwa mateso yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.
Aleluya.
Injili
Mk 14: 22-25Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni