Jumanne ya 7 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yak. 4: 1 – 10Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yenu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 55:6-10, 22Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Nikasema, ningekuwa na mbawa kama njiwa,
Ningerukia mbali na kustarehe.
Ningekwenda zangu mbali,
Ningetua jangwani.
K. Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Ningefanya haraka kuzikimbia
Dhoruba na tufani.
Ee Bwana uwaangamize, uzichafue ndimi zao.
K. Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Maana nimeona dhuluma na fitina katika mji
Machana na usiku huzunguka kutani mwake;
Uovu na taabu zimo ndani yake;
K. Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza,
Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
K. Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Shangilio la Injili
Ebr. 4:12Neno la Mungu li hai tena li nguvu, kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.
Injili
Mk. 9: 30 – 37Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. Akaketi chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote. Akatwaa k itoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, Mtu akimpokea motto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni