Sikukuu ya Mt. Mathia, Mtume
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Mdo. 1:15-17, 20-26Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; tena, Usimamizi wake autwae mwingine. Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu, kuanza tangu ubatizo wa Yohane, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.
Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya. Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 113:1-8Amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. au: Aleluya.
Aleluya.
Enyi watumishi wa Bwana, sifuni,
Lisifuni jina la Bwana.
Jina la Bwana lihimidiwe
Tangu leo na hata milele.
K. Amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. au: Aleluya.
Toka maawio ya jua hata machweo yake
Jina la Bwana husifiwa.
Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
K. Amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. au: Aleluya.
Ni nani aliye mfano wa Bwana,
Mungu wetu aketiye juu;
Anyenyekeaye kutazama,
Mbinguni na duniani?
K. Amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. au: Aleluya.
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
Amketishe pamoja na wakuu,
Pamoja na wakuu wa watu wake.
K. Amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. au: Aleluya.
Shangilio la Injili
Yn. 15 :16Ni mimi niliyewachagua ninyi, nikawaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kukaa.
Aleluya.
Injili
Yn. 15:9-17Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni