Jumatano ya 5 ya Pasaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo. 15:1-6Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana. Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.
Lakini baadhi. ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa. Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 122:1-5Nalifurahi waliponiambia, Na Twende nyumbani kwa Bwana.
Nalifurahi waliponiambia
Na twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu yetu imesimama
Ndani ya malango yako, ee Yerusalemu.
K. Nalifurahi waliponiambia, Na Twende nyumbani kwa Bwana.
Ee Yerusalemu uliyejengwa
Kama mji ulioshikamana,
Huko ndiko walikopanda kabila,
Kabila za Bwana.
K. Nalifurahi waliponiambia, Na Twende nyumbani kwa Bwana.
Ushuhuda kwa Israeli,
Walishukuru jina la Bwana.
Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,
Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.
K. Nalifurahi waliponiambia, Na Twende nyumbani kwa Bwana.
Shangilio la Injili
Yn. 10 :14Mimi ndimi mchungaji mwema, nao walio wangu nawajua, nao walio wangu wanijua mimi.
Aleluya.
Injili
Yn. 15 :1-8Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni