JUMA LA 3 LA PASAKA, JUMATANO
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Mdo 8:1-8Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.
Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.
Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 66:1-7Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote.
Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
Imbeni utukufu wa jina lake,
Tukuzeni sifa zake.
Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini.
K. Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote.
Nchi yote itakusujudia na kukuimbia,
Naam, italiimbia jina lako.
Njoni yatazameni matendo ya Mungu;
Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu.
K. Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote.
Aligeuza bahari ikawa nchi kavu;
Katika mto walivuka kwa miguu;
Huko ndiko tulikomfurahia.
Atawala kwa uweza wake milele;
Macho yake yawaangalia mataifa;
Waasio wasijitukuze nafsi zao.
K. Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote.
Shangilio la Injili
Yn. 10:27Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
Injili
Yn. 6:35-40Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni