Ijumaa ya Oktava ya Pasaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo 4:1-12Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 118:1-2, 4, 22-27Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Israeli na aseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
Wamchao Bwana na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
K. Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Jiwe walilolikataa waashi
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu.
Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana,
Tutashangilia na kuifurahia.
K. Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Ee Bwana, utuokoe, twakusihi;
Ee Bwana, utufanikishe, twakusihi.
Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana;
Tumewabarikia toka nyumbani mwa Bwana.
Bwana ndiye aliye Mungu, Naye ndiye aliyetupa nuru.
K. Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Injili
Yn 21:1-14Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni