Jumatatu ya 2 ya Kwaresima
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Dan. 9:4-10Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote uliowafukuza, kwa sababu ya makossa yao waliyokukosa. Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi. Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 79:8-9, 1, 13Usitutende sawasawa na hatia zetu, Ee Bwana.
Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,
Rehema zako zije kutulaki hima,
Kwa maana tumedhilika sana.
K. Usitutende sawasawa na hatia zetu, Ee Bwana.
Ee Mungu wokovu wetu utusaidie.
Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe, utughofiri dhambi zetu,
Kwa ajili ya jina lako.
K. Usitutende sawasawa na hatia zetu, Ee Bwana.
Kuugua kwake aliyefungwa na kuingie mbele zako.
Kwa kadiri ya uweza wa mkono wako
Uwahifadhi wana wa mauti.
Na sisi tulio watu wako, na kondoo za malisho yako,
Tutakushukuru milele;
Tutazisimulia sifa zako kizazi kwa kizazi.
K. Usitutende sawasawa na hatia zetu, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
Mt. 4:4Injili
Lk. 6:36-38Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni