Jumatano ya 32 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Hek. 6:1-11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 82:3-4,6-7Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi.
Mfanyieni hukumu maskini na yatima;
Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;
Mwokoeni maskini na mhitaji;
Mwopoeni mikoni mwa wadhalimu.
K. Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi.
Mimi nimesema, ndinyi miungu,
Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
Lakini mtakufa kama wanadamu,
Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
K. Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi.
Shangilio la Injili
Zab. 119:34Injili
Lk. 17:11-19Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya. Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, Imani yako imekuokoa.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni