Kumbukumbu ya Mtakatifu Klara, Bikira
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kum 4: 32-40Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa Bwana ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye. Kutoka mbinguni amekusikizisha sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonyesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake toka kati ya moto. Na kwa sababu aliwapenda baba zenu, kwa sababu hiyo aliwachagua wazao wao baada yao, akakutoa katika Misri kwa kuwako pamoja nawe, kwa uweza wake mwingi, ili kufukuza mbele yako mataifa, walio wakubwa, wenye nguvu kukupita wewe, ili kukuingiza, na kukupa nehi yao iwe urithi, kama ilivyo leo.
Kwa hivo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa Bwana ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine. Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo Bwana, Mungu wako, milele.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 77 :11-15, 20Ninayakumbuka matendo ya Bwana.
Nitayakumbuka matendo ya Bwana,
Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.
Pia nitaitafakari kazi yako yote;
Nitaziwaza habari za matendo yako.
K. Ninayakumbuka matendo ya Bwana.
Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu;
Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?
Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu;
Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.
K. Ninayakumbuka matendo ya Bwana.
Kwa mkono wako umewakomboa watu wako,
Wana wa Yakobo na Yusufu.
Uliwaongoza watu wako kama kundi,
Kwa mkono wa Musa na Haruni.
K. Ninayakumbuka matendo ya Bwana.
Shangilio la Injili
Mt. 4:4Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Aleluya.
Injili
Mt. 16: 24-28Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni