Alhamisi ya 17 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kut 40: 16-21, 34-38Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania. na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani. Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.
Hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani, wana wa Israeli wakaenda mbele katika safari zao zote, bali kama lile wingu halikuinuliwa, wakati ule hawakusafiri hata siku ile lilipoinuliwa tena. Kwa maana lile wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana. na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku. mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 84: 2-5, 7, 10Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Nafsi yangu imezionea shauku nyua za Bwana,
naam, na kuzikondea,
Moyo wangu na mwili wangu
Vinamlilia Mungu aliye hai.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Shomoro naye ameona nyumba,
Na mbayuwayu amejipatia kito,
Alipoweka makinda yake,
Kwenye madhabahu zako, Ee Bwana wa majeshi,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Heri wakaao nyumbani mwako,
Wanakuhimidi daima.
Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako,
Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.
Huendelea toka nguvu hata nguvu,
Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Hakika siku moja katika nyua zako
Ni bora kuliko siku elfu.
Ningependa kuwa bawabu
nyumbani mwa Mungu wangu,
K. Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Shangilio la Injili
1 Pet 1 : 25Neno la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.
Injili
Mt. 13: 47-53Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam. Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale. Ikawa Yesu alipoimaliza mifano hiyo, alitoka akaenda zake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni