Kumbukumbu ya Mtakatifu Martha
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kut. 24:3-8Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu. Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii. Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 50:1-2, 5-6, 14-15Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Mungu, Mungu Bwana, amenena, ameiita nchi,
Toka maawio ya jua hata machweo yake.
Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri,
Mungu amemulika.
K. Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Nikusanyieni wacha Mungu wangu,
Waliofanya agano nami kwa dhabihu.
Na mbingu zitatangaza haki yake,
Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.
K. Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru;
Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.
Ukaniite siku ya mateso;
Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.
K. Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Shangilio la Injili
Lk. 8:15Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao, hulisikia neno la Mungu na kulishika.
Aleluya.
Injili
Yn. 11:19-27Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; nave kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! unayasadiki hayo?
Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni