Alhamisi ya 15 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kut. 3:14-20Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.
Enenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri; Nami nimesema, Nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misrei na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, nchi ijaayo maziwa na asali. Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, Bwana, Mungu wa Waebrania, amekutana nasi; basi sasa twakuomba, tupe ruhusa twende mwendo wa siku tatu jangwani, ili tumtolee dhabihu Bwana, Mungu wetu. Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu. Nami nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 105:1, 5, 8-9, 24-27Bwana analikumbuka agano lake milele.
Aleluya.
Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake.
Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya,
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.
K. Bwana analikumbuka agano lake milele.
Analikumbuka agano lake milele;
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano alilolifanya na Ibrahimu,
Na uapo wake kwa Isaka.
K. Bwana analikumbuka agano lake milele.
Akawajalia watu wake wazae sana,
Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao.
Akawageuza moyo wawachukie watu wake,
Wakawatendea hila watumishi wake.
K. Bwana analikumbuka agano lake milele.
Shangilio la Injili
Zab. 19:8Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
Injili
Mt. 11:28 – 30Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni