DOMINIKA YA 14 YA MWAKA
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Zek. 9:9-10Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari za Amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 145:1-2, 8-11, 14, 17Nitalihimidi jina lako milele na milele.
Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza,
Nitalihimidi jina lako milele na milele.
Kila siku nitakuhimidi,
Nitalisifu jina lako milele na milele.
K. Nitalihimidi jina lako milele na milele.
Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema.
Bwana ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
K. Nitalihimidi jina lako milele na milele.
Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako.
K. Nitalihimidi jina lako milele na milele.
Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya kazi zako zote.
Bwana huwategemeza wote waangukao,
Huwainua wote walioinama chini.
K. Nitalihimidi jina lako milele na milele.
Somo la Pili
Rum. 8:9, 11-13Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
1Sam. 3:9; Yn. 6:68Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia;
Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Aleluya.
Injili
Mt. 11:25 – 30Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni