Jumatano ya 13 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa. 21:5, 8-20Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba. Yale maji yakaishaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja. Akaenda akakaa akimkabili, mbali i kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapazaza sauti yake, akalia.
Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa. Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana. Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 34 : 6-7, 9-13Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Maskini huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa na taabu zake zote.
Malaika wa Bwana hufanya kituo,
akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
K. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake,
yaani, wamchao hawahitaji kitu.
Wana-simba hutindikiwa, huona njaa,
bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu
chochote kilicho chema.
K. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Njoni, enyi wana, mnisikilize,
nami nitawafundisha kumcha Bwana.
Ni nani mtu yule apcndezwaye na uzima,
apendaye siku nyingi apate kuona mema?
K. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Shangilio la Injili
Zab. 119:105Neno lako ni taa ya miguu yangu,
na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
Injili
Mt. 8 :28-34Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe. Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini. Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote, na habari za wale wenye pepo pia. Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke mipakani mwao.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni