Ijumaa ya 12 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa 17:1,9-10,15-22Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake. Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema movoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa? Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako. Mungu akasema, sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake. Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu. Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao. Mungu akaacha kusema naye, akapanda kutoka kwa Ibrahimu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 128 : 1-5Tazama, atabarikiwa hivyo yule amchaye Bwana.
Heri kila mtu amchaye Bwana,
Aendaye katika nyia yake.
K. Tazama, atabarikiwa hivyo yule amchaye Bwana.
Taabu ya mikono yako hakika utaila;
Utakuwa heri, na kwako kwema.
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao.
Wanao Kama miche ya mizeituni
Wakiizunguka meza yako.
K. Tazama, atabarikiwa hivyo yule amchaye Bwana.
Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.
Bwana akubariki toka Sayuni;
Hone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako.
K. Tazama, atabarikiwa hivyo yule amchaye Bwana.
Shangilio la Injili
MT 11:25Nashukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi,
kwa kuwa mambo haya uliwaficha
wenye hekima na akili, ukawafunulia
watoto wachanga.
Aleluya.
Injili
Mt. 8:1-4Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni