KUMBUKUMBU YA MT. ALOIS GONZAGA (MTAWA)
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
2 Kor. 9:6 – 11Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu; mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 112:1 – 2, 4 – 9Heri mtu yule amchaye Bwana.
Heri mtu yule amchaye Bwana,
Apendezwaye sana na maagizo yake.
Wazao wake watakuwa hodari duniani;
Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
K. Heri mtu yule amchaye Bwana.
Nuru huwazukia wenye adili gizani;
Ana fadhili na huruma na haki.
K. Heri mtu yule amchaye Bwana.
Amekirimu, na kuwapa maskini,
Haki yake yakaa milele,
Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
K. Heri mtu yule amchaye Bwana.
Shangilio la Injili
Yak. 1:18Kwa kupenda kwake mwenyewe, Baba alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.
Aleluya.
Injili
Mt. 6:1-6, 16 – 18Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Tena mfungapo, msiwe kama wanfiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao; ili waonekane na watu kuwa nafunga, Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni